Kuhusu pombe

Kuendesha gari ukiwa umelewa:
Hatari na jinsi ya kukaa salama

Dru Jaeger
Imeandikwa na Dru Jaeger,
|
Des 16, 2025
|
6   dakika ya kusoma
Car Banner Image
1. Unachohitaji kujua kuhusu kunywa pombe na kuendesha gari 2. Jinsi unywaji pombe unavyoathiri vitendo na maamuzi tunayofanya 3. Viwango tofauti vya ulevi vinavyoruhusiwa kisheria 4. Matokeo ya kupitisha kiwango cha ulevi kinachoruhusiwa kisheria 5. Pima uelewa wako 6. Maswali Yanayoulizwa Sana 7. Kuanzia sasa: mwongozo na rasilimali 8. Mambo muhimu ya kuzingatia
Utangulizi

Hata kiasi kidogo cha pombe kinaweza kuathiri uamuzi wako na uwezo wa kuitikia haraka. Kuendesha gari baada ya kunywa pombe hakuhatarishi tu maisha yako mwenyewe, bali kunahatarisha pia usalama wa abiria wako, madereva wengine, watu wengine walio barabarani na watembea kwa miguu. Nchi nyingi zina kikomo cha juu zaidi cha pombe kinachoruhusiwa kisheria kwa kuendesha gari, lakini ukweli ni kwamba, pombe inaweza kuanza kuathiri tabia yako hata kabla ufikie kiwango cha ulevi kinachoruhusiwa kisheria.t. Bila kujali sheria inasema nini, chaguo salama zaidi huwa lilelile kila wakati: ikiwa unakunywa pombe yoyote, usiendeshe gari.

Kuhusu mwandishi
Dru Jaeger ni mwanzilishi mwenza wa Club Soda, mpango wa unywaji pombe unaozingatia watu, tena unaowawezesha watu kufanya maamuzi bora kuhusu pombe. Kupitia mipango anayotengeneza na kuongoza, Dru huwasaidia watu binafsi kujiamini katika maisha yao binafsi na ya kijamii. Yeye pia ni mwandishi wa kitabu cha Jinsi ya Kuwa Mnywaji Pombe Anayezingatia Wenzake (How to Be a Mindful Drinker).

1. Unachohitaji kujua kuhusu kunywa pombe na kuendesha gari

Ili kuwaweka watumiaji wote wa barabara kuwa salama, nchi nyingi huweka vikomo vya kisheria vya kiasi cha pombe unachoweza kuwa nacho kwenye mfumo wako unapoendesha gari (1), lakini kumbuka kuwa hii ni miongozo tu, wala si uhakikisho. Hata kama hujafikia kiwango cha ulevi kinachoruhusiwa, uratibu wako na muda wa kuitikia unaweza kuathiriwa. Ukipita kiwango cha ulevi kinachoruhusiwa, unaweza kutarajia kutozwa faini kubwa, leseni kusitishwa, au hata kifungwa jela. Njia bora ya kupunguza hatari yako ya kupata ajali ya barabarani na kusababisha madhara kwako au kwa wengine ni kutokunywa pombe ikiwa unaendesha gari. Ikiwa umekunywa pombe yoyote, daima chagua njia salama ya kurudi nyumbani, kama vile usafiri wa umma au kuagiza teksi.

2. Je, unywaji pombe unaathiri vipi vitendo na maamuzi yetu?

Pombe inapofyonzwa ndani ya miili yetu, baadhi yake hufika kwenye ubongo wetu, ambapo inaanza mara moja kuathiri jinsi tunavyochakata taarifa na kukabiliana na kinachotokea karibu nasi. (2) Kadiri tunavyoendelea kunywa, ndivyo kiwango cha pombe kwenye damu (BAC) kinaongezeka, na ndivyo athari kwenye ubongo wetu inavyoongezeka. (3) Hii husababisha tujibu mambo polepole, uratibu uliopunguzwa, na uamuzi mbaya.

BAC, inayopimwa kwa miligramu za pombe kwa lita moja ya damu, ni kipimo kinachotambulika na watu wengi cha kiasi ambacho umekunywa na jinsi uwezo wako wa kimwili na kiakili unavyoweza kuathiriwa baada ya kunywa pombe. Ni kiwango kinachotumiwa na wenye mamlaka ili kubaini ikiwa mtu anafaa kuendesha gari kwa mujibu wa sheria. Lakini ukweli ni kwamba, pombe inaweza kuanza kuathiri tabia yako hata kabla ufikie kiwango cha ulevi kinachoruhusiwa kisheria.

Muda wa kucheza: dakika 2

Muda wa kutazama: dakika 10

Did you know Image

Je, wajua?

Je, unajua kwamba takriban 35% ya vifo vya barabarani ulimwenguni vinahusiana na pombe? (4)

4.  Je, nini kitatokea ikiwa umevuka kiwango cha ulevi kinachoruhusiwa kisheria

Njia sahihi pekee ya kujua BAC yako ni kufanya kipimo. Vyombo vya kutekeleza sheria kwa kawaida hupima BAC kupitia vipimo vya pumzi kando ya barabara au kwa kuchukua sampuli za damu. Ni rahisi: ukipatikana kuwa umevuka kikomo, basi umevunja sheria. Na matokeo yanaweza kuwa makubwa. Katika baadhi ya maeneo, wakosaji ambao wamewahi kupatikana na hatia hapo awali wanaweza kuhitajika kusakinisha kifaa cha kupima pombe katika pumzi kwenye gari lao, na kifaa hiki huzuia injini kuwaka, pombe ikigunduliwa kwenye pumzi zao.

Ingawa kuna uhusiano dhahiri kati ya kiasi cha pombe unachokunywa na BAC yako, kiwango chako halisi kinategemea mambo mbalimbali binafsi, kama vile uzito, umri, jinsia na umetaboli. Jinsi ulivyokunywa pombe haraka kunaweza pia kuathiri viwango vya pombe.

Car keys and a glass of alcohol with a warning symbol, indicating the danger of drinking and driving.
Pima uelewa wako

Jaribu ujuzi wako kwa maswali yetu hapo chini, bofya kufichua jibu na uone kama ulikuwa sahihi.

Swali: Kweli au Si Kweli: Ilimradi nibaki chini ya kiwango halali cha BAC, uendeshaji wangu hautaathirika vibaya ninapokunywa pombe.

Jibu: SI KWELI

Kunywa pombe kunaweza kuathiri uendeshaji wako hata kabla ufikie kiwango cha BAC kinachoruhiswa kisheria. Ingawa kiwango cha athari kinategemea kiasi cha pombe ulichokunywa, chaguo salama zaidi ni kutothubutu kunywa pombe na kuendesha gari.

Swali: Ni lipi kati ya yafuatayo ambalo ni kweli?

Kiwango cha kisheria cha BAC cha kuendesha gari ni:

A: 0.02mg/dL 
B: 0.05mg/dL 
C: Ni tofauti kulingana na nchi

Jibu: C Ni tofauti kulingana na nchi

Nchi tofauti huweka viwango tofauti vya BAC vya kunywa pombe na kuendesha gari. Ili kujua kiwango kinachoruhusiwa kisheria katika nchi yako, angalia:

https://iard.org/science-resources/detail/Blood-Alcohol-Concentration-(BAC)-Limits

Swali: Kweli au Si Kweli: Viwango vya BAC vinaweza kuwa tofauti kwa madereva wenye uzoefu na wanaojifunza.

Jibu: KWELI

Baadhi ya nchi huweka kiwango cha chini cha BAC kwa madereva wasio na uzoefu, madereva wachanga, na wanaojifunza kuendesha gari. Katika baadhi ya matukio, madereva hawa huadhabiwa vikali kwa kunywa pombe.

Swali: Ni kauli ipi iliyo sahihi: Madhumuni ya vifaa vya kupima pombe katika pumzi ni:

1. Kukusaidia kuwasha gari lako kiotomatiki.
2. Kuzuia kuendesha gari ikiwa umekuwa ukinywa pombe.
3. Kufanya iwe vigumu kwa gari lako kuibiwa

Jibu: 2. Kuzuia kuendesha gari ikiwa umekuwa ukinywa pombe.

Vifaa vya kupima pombe katika pumzi vinahitaji kipimo cha pombe ili uweze kuwasha gari lako na hutumiwa kuzuia wakosaji ambao wamewahi kupatikana na hatia hapo awali kunywa pombe na kuendesha gari.

Maswali Yanayoulizwa Sana
Je, ninaweza kunywa vinywaji visivyo na kileo ninapoendesha gari?

Ndiyo.
Vinywaji visivyo na kileo (kwa mfano, bia isiyo na pombe) inaweza kuwa na kiasi kidogo cha pombe, lakini, kwa vyovyote vile, kiwango hicho huwa kidogo sana na hakitaathiri uendeshaji wako. Ikiwa unapanga kuendesha gari, vinywaji visivyo na kileo ni chaguo zuri badala ya vyenye kileo.

Je, ninapaswa kusubiri kwa muda gani kabla ya kuendesha gari baada ya kunywa pombe?

Ni bora kuepuka kuendesha gari baada ya kunywa pombe. Lakini ikiwa lazima uendeshe gari, unapaswa kusubiri angalau saa moja kabla ya kufanya hivyo.  Kunywa maji na vinywaji visivyo na kileo kutakusaidia kurejesha maji mwilini.  Hata hivyo, ikiwa umekunywa vinywaji kadhaa kwa muda mfupi, chaguo salama zaidi ni kutumia usafiri mbadala, kwani uko katika hatari kubwa ya kupata ajali ya barabarani kwa saa kadhaa baada ya kunywa pombe.  

Je, unywaji pombe huathiri vipi kuendesha gari? 

Kunywa pombe hupunguza muda wako wa kuitikia, jinsi unavyoona mazingira yako, na uwezo wako wa kufanya maamuzi na kufanya hivyo haraka. Ustadi wako wa kuendesha gari huendelea kupungua kadiri kiasi cha pombe katika damu yako kinavyoongezeka, lakini hata kinywaji kimoja kinaweza kuathiri uwezo wako wa kawaida wa kuendesha gari na kukabiliana na ulimwengu unaokuzunguka.  

Je, kunywa kinywaji kimoja au chini ya kinywaji kimoja kunaweza kuathiri uendeshaji wako? 

Kiasi chochote cha pombe kinaweza kuathiri uwezo wako wa kuendesha gari. Kadiri unavyozidi kunywa pombe, ndivyo unavyoendelea kuathiri uwezo wako. Jinsi kinywaji kimoja au kiasi kidogo kuliko kinywaji kimoja kinavyoweza kukuathiri kunategemea wewe ni nani -- umri na uzito wako, ikiwa umekula, na ikiwa unatumia dawa zinazoweza kuathiriwa na pombe. Njia salama zaidi unapokuwa umekunywa pombe ni kutoendesha gari, na kutokunywa pombe unapoendesha gari. 

Marejeleo

(1) Muungano wa Kimataifa wa Unywaji Pombe kwa Kuwajibika (IARD), Viwango vya Ukolezi wa Pombe katika Damu (BAC). 2020, IARD: Washington, DC.

(2) Abrahao, K.P., A.G. Salinas, na D.M. Lovinger, Alcohol and the Brain: Neuronal Molecular Targets, Synapses, and Circuits. Neuron, 2017. 96(6): uk. 1223-1238.

(3) Alcohol.org.nz. Kiwango cha pombe katika damu. 2020; Inapatikana kutoka:

(4) Ripoti ya hali ya kimataifa kuhusu usalama barabarani 2018. Geneva: Shirika la Afya Duniani; 2018. Leseni: CC BY-NC-SA 3.0 IGO.