Ni nini athari za pombe kwenye afya ya akili?

Inategemea mambo mengi , kama vile unakunywa kiasi gani na hali yako ya asili ya akili, na kuna athari za muda mfupi na za muda mrefu za kuzingatia.
Ni nini athari za pombe kwenye afya ya akili?
Ni nini athari za pombe kwenye afya ya akili?

Pombe ni kinywaji kinachoathiri ubongo wako ubongo wako na kemikali zinazohusika moja kwa moja na matendo na mhemko wako (1). Kwa kifupi ni kuwa, unywaji wa kistarabu unaweza kukufanya ukajisikia vizuri Watu wengi hufurahia kunywa kwa sababu inawapa raha na inaweza kuongeza uchangamfu kwenye mkusanyiko wa kijamii (2).

Hata hivyo, unapo kunywa zaidi, athari mbaya za pombe huchukua nafasi. Hali yako nzuri inaweza kugeuka haraka, na unaweza kuwa na huzuni au kufadhaika Unywaji wa muda mrefu, unaweza kuwa na athari ya kudumu kwa afya yako ya akili (3). Watu wengine wanaweza kunywa ili kupunguza mfadhaiko au wasiwasi na kutumia pombe kupunguza hisia zao (4, 5). Baada ya muda, wanaweza kuanza kunywa zaidi na wanahitaji pombe zaidi ili kupata matokeo wanayoyataka . Lakini kunywa kupita kiasi kunaweza kusababisha mafadhaiko na wasiwasi kuwa mbaya zaidi na kusababisha shida za ziada za afya ya akili (6, 7).

Hali ya afya ya akili na Matatizo ya Matumizi ya Pombe yanahusiana sana

Uchunguzi wa kisayansi unaonyesha kuwa kunywa kupita kiasi kunahusiana sana na mfadhaiko (6), wasiwasi (8), psychosis (9) na ugonjwa wa bipolar (10) - na inaweza pia kuongeza hatari ya kujiua (11). Watu wengi ambao wanakabiliwa na shida hizi ni wanywaji pombe sana na wanaweza kugundulika kuwa na Shida ya Matumizi ya Pombe (AUD), au utegemezi. Kwa kweli, AUD yenyewe inachukuliwa kama hali ya afya ya akili na inahitaji msaada wa wataalamu (12).

Kunywa wakati unatumia dawa kunaweza kuwa na athari mbaya kwa afya yako ya akili

Mchoro wa matumizi tofauti tofauti ya madawa
Mchoro wa matumizi tofauti tofauti ya madawa

Watu wengi ambao wana matatizo ya ya afya ya akili hutumia madawa kutuliza mihemko na tabia zao. Pombe inaweza kuingiliana na dawa hizi na zingine, kwa hivyo watu wanaotumia kwa ujumla wanashauriwa wasinywe (13, 14). Pombe inaweza kuingiliana na dawa hizi na zingine, kwa hivyo watu wanaotumia kwa ujumla wanashauriwa wasinywe (15). Muingilingiliano kati ya pombe na dawa za kulevya, iwe ni halali au la, inaweza kubadilisha au kuzidisha athari za zote mbili na inaweza kusababisha kifo.

Kunywa kwa 'kujitibu' na kubadilisha mhemko wako sio wazo nzuri kamwe. Ikiwa unapata shida kukabiliana na shida ya afya ya akili, ni bora kutafuta msaada wa wataalamu - nambari za msaada na rasilimali zingine pia zinapatikana. Vivyo hivyo, ikiwa una wasiwasi juu ya kunywa kwako mwenyewe au kwa wengine na athari zake kwa afya ya akili, mtaalamu wa afya anaweza kusaidia kuamua kiwango chako cha hatari na njia sahihi zaidi au matibabu.

Taarifa hizi zinaweza kuwa za msaada kwa mtu yeyote aliyepo nchini Kenya au Tanzania.

References
  1. Abrahao, K.P., A.G. Salinas, and D.M. Lovinger, Alcohol and the Brain: Neuronal Molecular Targets, Synapses, and Circuits. Neuron, 2017. 96(6): p. 1223-1238.
  2. Sayette, M.A., The effects of alcohol on emotion in social drinkers. Behav Res Ther, 2017. 88: p. 76-89.
  3. Mental Health Foundation. Alcohol and mental health. 2020; Available from:
  4. Hunt, G.E., et al., Prevalence of comorbid substance use in major depressive disorder in community and clinical settings, 1990-2019: systematic review and meta-analysis. Journal of Affective Disorders, 2020. 266: p. 288-304.
  5. Becker, H.C., Influence of stress associated with chronic alcohol exposure on drinking. Neuropharmacology, 2017. 122: p. 115-126.
  6. Boden, J.M. and D.M. Fergusson, Alcohol and depression. Addiction, 2011. 106(5): p. 906-14.
  7. Li, J., et al., Effect of alcohol use disorders and alcohol intake on the risk of subsequent depressive symptoms: a systematic review and meta-analysis of cohort studies. Addiction, 2019. Published early online 16 January 2020.
  8. Thibaut, F., Anxiety disorders: a review of current literature. Dialogues Clin Neurosci, 2017. 19(2): p. 87-88.
  9. Stankewicz, H.A., J.R. Richards, and P. Salen, Alcohol Related Psychosis, in StatPearls. 2020, StatPearls Publishing, Copyright © 2020, StatPearls Publishing LLC.: Treasure Island (FL).
  10. Farren, C.K., K.P. Hill, and R.D. Weiss, Bipolar disorder and alcohol use disorder: a review. Curr Psychiatry Rep, 2012. 14(6): p. 659-66.
  11. Borges, G., et al., A meta-analysis of acute use of alcohol and the risk of suicide attempt. Psychol Med, 2017. 47(5): p. 949-957.
  12. American Psychiatric Association (APA), Diagnostic and statistical manual of mental disorders (5th ed.). 2013, APA: Arlington, VA.
  13. (NIAAA), N.I.o.A.A.a.A., Harmful interactions: mixing alcohol with medicines., NIAAA, Editor. 2014, NIAAA: Gaithersburg, MD.
  14. Linnoila, M., M.J. Mattila, and B.S. Kitchell, Drug interactions with alcohol. Drugs, 1979. 18(4): p. 299-311.
  15. Meier, P.J., [Alcohol, alcoholism and drugs]. Schweiz Med Wochenschr, 1985. 115(50): p. 1792-803.