Vinywaji vingine kama pombe kali ni 'ngumu' na vingine kama bia ni 'laini'.
Uwongo. Pombe kali ina kilevi kwa wingi n kuliko baadhi ya waini nmbazo zina kilevi kuliko baadhi ya bia Lakini, licha ya mitizamoi kadhaa maarufu, hakuna kitu kama pombe ngumu na 'laini', au, kama inavyoitwa katika maeneo mengine, vinywaji vya 'moto' na 'baridi'. Bia, waini , pombe kali zilizosafishwa na vinywaji vyenye mchanganyiko vyote vina aina moja ya pombe inayoitwa ethanoli, wambayo inawajibika kwa athari unazohisi bila kujali unachokunywa.
Nchi zote zinatumia 'kipimo' sawa ili kuhakikisha kuwa uhudumiaji wa bia, waini na pombe kali ni sawa.
Siyo kweli . Hakuna ukubwa wa kawaida wa kinywaji kote ulimwenguni. Wakati ufafanuzi nchini Uingereza ni gramu nane za ethanoli (1), nchi tofauti hutumia ufafanuzi tofauti, na ukubwa wa vitengo vingine vina gramu 14 za ethanoli (2). Walakini, ndani ya kila nchi, huduma ya kawaida ya bia, divai au pombe hufafanuliwa kwa njia ile ile. Kwa kawaida, , vinywaji mara nyingi havihudumiwa kwa ukubwa wa kawaida, lakini dhana ya kipimo cha kawaida ni muhimu.
Athari ya pombe kwako inategemea ikiwa unakunywa bia, waini au pombe kali.
Siyo kweli Bia, waini i na pombe kali zote zina aina moja ya kilevi , ethanoli, ambayo ina athari sawa kwa mwili wako bila kujali unachokunywa. Jambo muhimu ni kiasi gani cha ethanol unachokunywa na jinsi unavyokunywa kwa haraka. Pombe iliyo na kiwango kikubwa cha kilevi, huudumiwa kwa kipimo kidogo , Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa hii siyo kila mara humaanisha namna kinywaji kinavyohudumiwa. Kwa mfano unaweza kuwa unakunywa nyumbani kwenye glasi ambayo haipo kwenye saizi ya kawaida.
Kiasi inaweza kukusaidia kuhakikisha kuwa unywaji wako unakaa ndani ya miongozo iliyopendekezwa na haikudhuru.
Kweli. Miongozo ya unywaji ya Uingereza hutoa ushauri juu ya viwango na mifumo ya kunywa kwa kutumia vitengo kama kumbukumbu (3). Mwongozo wa Mganga mkuu wa Uingereza kwa wanaume na wanawake sio kunywa zaidi ya vipimo14 kwa wiki mara kwa mara ili kupunguza hatari zozote za kiafya kutokana na pombe. Kuelewa dhana ya kitengo inaweza kukusaidia kuhusisha unywaji wako mwenyewe na mapendekezo ambayo yanaambatana na mtindo sawa wa maisha. Kunywa zaidi ya miongozo iliyopendekezwa kunaweza kuongeza uwezekano wa kupata madhara.