Kunywa pombe kunaathiri vipi ubongo wako, mfumo wa umeng'enyaji chakula, na moyo?

Kunywa pombe kutaathiri mifumo ya mwili wako [1], na kiwango cha athari kinategemea mambo mengi. Haya ndiyo unayopaswa kujua.

Mwanamke aliyevaa fulana ya michezo ya kijani kibichi yuko nje kwenye mandhari ya majani. Anageuza uso wake juu kuelekea kwenye jua.
 - Unywaji unaathirije ubongo, ini na moyo?

Mojawapo ya viungo vya kwanza kuathiriwa na unywaji wako ni ubongo

Hakuna watu wawili watakaopata athari sawa kutokana na kunywa pombe lakini kwa kawaida watahisi athari zake ndani ya dakika chache. Ethanoli inapoingia kwenye ubongo wako, huingiliana na kemikali na mikondo ya mawasiliano inayodhibiti hisia na hali yako ya roho, jinsi unavyoitikia raha na maumivu, na kudhibiti uratibu, mwendo na hata pumzi yako [2].

Kunywa kiasi kunaweza kukufanya uwe huru zaidi na utulie, lakini kadiri unavyokunywa zaidi, ndivyo pombe inavyozidi kupunguza uwezo wako wa kufanya kazi vizuri. Ukikunywa kupita kiasi kwa muda mfupi, unaweza kupoteza fahamu. Katika hali mbaya zaidi, watu wanaolewa kupita kiasi wanaweza kuingia kwenye koma na hata kuacha kupumua [3]. Majibu haya yote yanahusisha ubongo wako.

Utafiti umeonyesha kuwa unywaji mzito kupita kiasi kwa kipindi kirefu unaweza pia kubadilisha muundo wa ubongo [4]. Tofauti na baadhi ya viungo vingine, ubongo hauzalishi upya, hivyo uharibifu wowote hauwezi kurekebishwa. Hii pia ni sababu moja kwa nini kunywa pombe ukiwa na umri mdogo si wazo zuri hata kidogo. Kwa kuwa ubongo wa vijana bado unakua, pombe inaweza kuvuruga jinsi miunganisho ya ubongo inavyoundwa, hususan ile inayohusika na ujifunzaji na kumbukumbu [5, 6].

Baadhi ya tafiti za kisayansi zimeonyesha kuwa kwa baadhi ya watu wazee, unywaji wa wastani unaweza kuwa na athari chanya kwa jinsi ubongo unavyofanya kazi, kuboresha uwezo wa kufikiri na kumbukumbu, na kupunguza kasi ya upungufu wa akili unaoonekana kadri umri unavyoongezeka [7-9].

Hata hivyo, athari hizi hazimhusu kila mtu, na haupaswi kuanza kunywa kwa sababu za kiafya. Ni mtaalamu wa afya aliyehitimu pekee anayeweza kukupa ushauri kulingana na mtindo wako wa unywaji pombe, afya, na mtindo wako wa maisha. Watu wazima wanaweza kuhitaji ushauri maalumkuhusu unywaji pombe na athari zake.

Ni muhimu kukumbuka kwamba athari za kiafya za unywaji pombe ni zilezile bila kujali ikiwa umechagua bia, mvinyo, au pombe kali. Zote zina athari sawa kwenye ubongo wako na kwenye viungo na mifumo mingine mwilini mwako, kulingana na kiasi unachokunywa. Kwa madhumuni ya afya, pombe ni pombe.

An older man is wearing a bright red sports jacket, and smiling.  He is outside against a leafy background.
 - Mchoro wa kiwiliwili cha binadamu na tumbo iliyochorwa wazi

Ini ni sehemu kuu ya mwili wako ya kusafisha pombe

Ini ni sehemu ya mfumo wako wa umeng'enyaji na lina jukumu la msingi la kumeng'enya pombe nyingi unayokunywa [21]. Ethanoli iliyomo kwenye kinywaji chako hubadilishwa kwanza kuwa dutu inayoitwa asetaldehaidi, ambayo ni sumu kwa mwili, hivyo huvunjwavunjwa haraka na kuondolewa kupitia mkojo.

Unywaji pombe kupindukia kutaathiri ini lako [22]. Enzaimu zilizopo kwenye ini zinaweza kuchakata takribani kinywaji kimoja kwa kila saa; unywaji wa zaidi na kwa kasi kubwa husababisha asetaldehaidi kujikusanya na kubaki mwilini kwa muda, na hivyo kusababisha uharibifu. Watu ambao hunywa sana kwa muda mrefu huvimbiwa ini na hali inayoitwa cirrhosis ambapo tishu za makovu huongezeka na huzuia ini kufanya kazi kwa kawaida.

Jinsi pombe inavyoathiri ini lako pia inategemea mambo mengine [23]. Utafiti unaonyesha kuwa kunenepa sana na kutumia dawa fulani kunaweza kuharibu ini lako, kuongeza uvimbe na uwezekano wa kupata acetaldehyde. Ikiwauna wasiwasi juu ya athari za kunywa kwako kwenye afya ya ini lako, au jinsi inavyoweza kuingiliana na dawa, kushauriana na mtaalamu wako wa afya ni hatua bora ya kupata ushauri sahihi ambao’ unakufaa.

An older lady wearing sportswear, and a towel around her neck, is outside exercising.  She is smiling while listening to music.
 - Mchoro wa kiwiliwili cha binadamu na moyo iliyochorwa wazi

Kunywa pombe kuna athari mbalimbali kwa moyo wako kulingana na jinsi unavyokunywa na jinsi ulivyo

Kunywa pombe kupita kiasi sio kuzuri kwa moyo [24]. Inaweza kusababisha mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, yanayojulikana kama arrhythmia [25], hata baada ya kipindi kimoja cha kunywa pombe nyingi. Huenda umesikia kuhusu ‘sindromu ya moyo wa likizo’, ambapo midundo ya vyumba vya moyo inavyopaswa kushirikiana huvurugika baada ya unywaji wa kupita kiasi (na ulaji), mara nyingi wakati wa sherehe za likizo [26]. Unaweza kuhisi kichwa chepesi, kizunguzungu, na kukosa pumzi. Matukio ya unywaji mzito mara kwa mara yanaweza kuongeza hatari ya matatizo ya muda mrefu kama kushindwa kwa moyo na kiharusi [27, 28]. Watu ambao wana matatizo fulani ya moyo au historia ya familia ya ugonjwa wa moyo wanaweza kushauriwa wasinywe pombe kamwe.

Hata hivyo, utafiti uliofanywa kwa miongo kadhaa unaunga mkono wazo kwamba kwa baadhi ya watu wa umri wa kati na wazee, unywaji wa wastani unaweza kuwa mzuri kwa moyo [28]. Ikilinganishwa na watu wasiokunywa , wale wanaokunywa kidogo au kwa wastani wana kiwango cha chini cha kolesteroli na kuhifadhiwa kidogo kwenye mishipa yao ya damu [29], na kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi. Lakini hili halihusu kila mtu kwa usawa. Sababu nyingine pia zinahusika, zikiwemo umri, jinsia, na afya kwa ujumla. Hata kiasi kidogo cha pombe kinaweza kuwa hatari kwa watu wanaotumia dawa fulani au wana matatizo mengine ya kiafya.

Katika miaka ya hivi karibuni, wanasayansi wengine wamehoji faida za unywaji wa wastani kwa afya ya moyo, wakihoji mapungufu yanayowezekana katika baadhi ya tafiti muhimu [30-32]. Hata hivyo, pale ambapo hakuna mgongano kati ya wanasayansi ni kuhusu athari ambazo unywaji kupita kiasi unaweza kuwa nazo kwa moyo wako. Unywaji wa pombe kupita kiasi kwa muda mfupi na unywaji mzito kwa kipindi kirefu unaweza kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo. Kwa sababu athari za unywaji pombe ni tofauti kwa kila mtu, ni muhimu ’ kushauriana na mtaalamu wa matibabu ikiwa una maswali kuhusu unywaji wako na athari zake kwa moyo wako.

Unywaji pombe kupita kiasi unaweza kuvuruga uwiano na utendaji wa utumbo wako
Dk Megan Rossi (PhD, RD)

Pombe huathiri mikrobiomu ya mfumo wako wa mmeng’enyo, na unywaji wa pombe kupita kiasi unaweza kuchangia uvimbe katika mwili mzima.

Ikiwa hukujua, kudumisha utumbo wenye afya hakusaidii tu umeng'enyaji sahihi, lakini pia huathiri mfumo wako wa kinga (na karibu 70% ya mfumo wako wa kinga unaishi huko), kukusaidia kupambana na maambukizi na kuzuia magonjwa mengine, na pia kuchangia maisha yako marefu, ustawi wa akili na mengi zaidi . Hii inahusisha ‘ mikrobiomu ya ’ , mfumo wa matrilioni za viumbe vidogo vidogo vinavyofanya kazi kudumisha afya yako na utendaji wako, na uhusiano wake na karibu kila mfumo na kazi katika mwili.

Mikrobiomu ya mfumo wa mmeng’enyo ina jukumu kama kusaidia kudhibiti uvimbe na kuvurugausawa wa mfumo wa mmeng’enyo wako katika utumbo wako(mlingano) kunakuwa na athari nyingi kwenye afya yako kwa ujumla.

Unywaji wa kupita kiasi ndio sababu moja muhimu ya kuvuruga ayoni na kuruhusu bakteria zaidi wenye sifa za kuleta uvimbe kukua, na kupunguza bakteria zinazojulikana kwa sifa zao za kupunguza uvimbe [11]. Athari za muda mfupi ni dhahiri – unaweza kupata tindikali , kichefuchefu/kutapika, kutokwa na damu au kuhara [12, 13 14]. Kichwa kuuma na dalili nyingine za kizunguzungu ndizo dalili za kwanza na dhahiri zaidi za uvimbe baada ya unywaji mzito.

Kwa muda mrefu, unywaji kupita kiasi hufanya mikrobiomu ya mfumo wako wa mmeng’enyo kuwa na utofauti mdogo, na kuongeza hatari ya utumbo kuvuja (leaky gut) na dalili za utumbo wenye msongo (irritable bowel syndrome) [15, 16]. Pia imehusishwa na kuongeza hatari ya kuwa na matatizo yanayohusiana na kinga ya mwili, matatizo ya kupoteza ufanisi wa nevana baadhi ya aina za saratani [17, 18, 19]. Yote haya yanahusisha kupungua kwa uwezo wa mwili kupambana na uvimbe.

Habari njema ni kwamba mikrobiomu ya mfumo wa mmeng’enyo ni yenye ustahimilivu na inaweza kurejeshwa katika hali yenye afya kwa kupunguza unywaji wa pombe na kubadilisha lishe yako kwa kuzingatia utofauti wa mimea kulingana na kile ambacho Dkt. Megan Rossi (PhD, RD) anaita Super Six (matunda, mboga, nafaka nzima, maharagwe, karanga na mbegu, pamoja na mimea na viungo) kuruhusu mikrobiomu ya mfumo wa mmeng’enyo kupona [20]. Aina zote za vinywaji vya pombe huchangia kuvimba wakati vinatumiwa zaidi na vinaweza kuathiri vibaya mikrobiomu ya utumbo.,

Dk Megan Rossi (PhD, RD), mwanzilishi wa The Gut Health Doctor alisema: “Pombe inazungumza kikamilifu na mikrobiumi zako za tumbo na inaweza kubadilisha mchanganyiko wa kipekee wa vijidudu katika njia yako ya umeng'enyaji, ikimaanisha hata vinywaji vichache vinaweza kubadilisha jinsi utumbo wako unavyofanya kazi. Wakati uwiano wa vijidudu unavyobadilika, hivyo pia unavyoweza kubadilika upitishaji wa utumbo (utumbo kuvuja), uvimbe, mmeng’enyo na hata tabia za haja kubwa. Huhitaji kuacha pombe kabisa ili kusaidia afya yako ya utumbo, lakini kufanya uchaguzi sahihi kunaweza kuleta mabadiliko halisi. Kwa mfano, kupunguza kiasi cha unywaji pombe kwa ujumla, kubadilishana na vinywaji visivyo na pombe, kuongeza matunda ya beri yaliyogandishwa pamoja na maji yenye viputo badala ya vichanganyio vyenye sukari nyingi au vile vya lishe vinapotumika na vileo, kuchagua chaguzi zilizo na kiwango cha juu cha polyphenol (viambato vya mimea vinavyopendwa na vijidudu vya utumbo) kama vile divai nyekundu, bia nyeusi na whisky yenye tangawizi, kuepuka kunywa ukiwa tumbo tupu, kuulisha vema mfumo wa vijidudu tumboni kwa vyakula vya mimea vyenye wingi wa nyuzinyuzi kabla na baada ya unywaji wa pombe, pamoja na kunywa maji ya kutosha, kunasaidia yote. Zaidi ya hayo, kuwa makini na jinsi mwili wako unavyoitikia pombe kwa kuangalia jinsi tumbo lako linavyojisikia baada ya kunywa. Kupitia uelewa huu ulioongezeka na kwa kuchukua hatua ndogo ndogo za kuusaidia utumbo wako, unaweza kufurahia matukio ya kijamii bila kuathiri afya ya utumbo wako ya muda mrefu.”

References
  1. National Institute on Alcohol Abuse and Alcoholism (NIAAA). Alcohol's Effects on the Body. 2020; Available from:
  2. Abrahao, K.P., A.G. Salinas, and D.M. Lovinger, Alcohol and the Brain: Neuronal Molecular Targets, Synapses, and Circuits. Neuron, 2017. 96(6): p. 1223-1238.
  3. National Health Service (NHS). Alcohol poisoning. 2019; Available from:
  4. Sullivan, E.V., R.A. Harris, and A. Pfefferbaum, Alcohol's effects on brain and behavior. Alcohol Res Health, 2010. 33(1-2): p. 127-43.
  5. Spear, L.P., Effects of adolescent alcohol consumption on the brain and behaviour. Nat Rev Neurosci, 2018. 19(4): p. 197-214.
  6. Squeglia, L.M. and K.M. Gray, Alcohol and Drug Use and the Developing Brain. Curr Psychiatry Rep, 2016. 18(5): p. 46.
  7. Sinforiani, E., et al., The effects of alcohol on cognition in the elderly: from protection to neurodegeneration. Funct Neurol, 2011. 26(2): p. 103-6.
  8. Rehm, J., et al., Alcohol use and dementia: a systematic scoping review. Alzheimers Res Ther, 2019. 11(1): p. 1.
  9. Brust, J.C., Ethanol and cognition: indirect effects, neurotoxicity and neuroprotection: a review. Int J Environ Res Public Health, 2010. 7(4): p. 1540-57.
  10. van den Berg, H., van der Gaag, M., & Hendriks, H.. Influence of lifestyle on vitamin bioavailability. Int J Vitam Nut. Res, 2002. 72: 53–59.
  11. Engen, P.A. et al., The gastrointestinal microbiome: Alcohol effects on the composition of intestinal microbiota. Alcohol Res, 2015. 37(2): p. 223-36.
  12. Bala, S. et al., Acute binge drinking increases serum endotoxin and bacterial DNA levels in healthy individuals. PLoS ONE, 2014. 9(5): p. e96864.
  13. Stadlbauer, V., A. Horvath, & I. Komarova, A single alcohol binge impacts on neutrophil function without changes in gut barrier function and gut microbiome composition in healthy volunteers. PLoS ONE, 2019. 14(2): p. e0211703.
  14. Yegen, B.C., Lifestyle and peptic ulcer disease. Curr Pharm Des, 2018. 24(18): p. 2034-2040.
  15. Calleja-Conde, J. et al., The immune system through the lens of alcohol intake and gut microbiota. Int J Mol Sci, 2021. 22(14): p. 7485;
  16. Manos, J. The human microbiome in disease and pathology. APMIS, 2022. 130(12): p. 690-705.
  17. Jain, A., S. Madkan, & P. Patil, The role of gut microbiota in neurodegenerative diseases: Current insights and therapeutic implications. Cureus, 2023. 15(10): p. e47861.
  18. Sepich-Poore, G.D. et al., The microbiome and human cancer. Science, 2021. 37(6536): p. eabc4552;
  19. Cullin, N. et al. Microbiome and cancer. Cancer Cell, 2021. 39(1):p. 1317-1341.
  20. Gagliardi, A. et al., Rebuilding the gut microbiota ecosystem. Int J Environ Res Public Health, 2018. 15(8):1679.
  21. Cederbaum, A.I., Alcohol metabolism. Clin Liver Dis, 2012. 16(4): p. 667-85.
  22. Rocco, A., et al., Alcoholic disease: liver and beyond. World J Gastroenterol, 2014. 20(40): p. 14652-9.
  23. Roerecke, M., et al., Alcohol consumption and risk of liver cirrhosis: A systematic review and meta-analysis. Am J Gastroenterol, 2019. 114(10): p. 1574-1586.
  24. Mostofsky, E., et al., Alcohol and immediate risk of cardiovascular events: A systematic review and dose-response meta-analysis. Circulation, 2016. 133(10): p. 979-87.
  25. Wong, C.X., S.J. Tu & G.M. Marcus, Alcohol and arrhythmias. JACC Clin Electrophysiol, 2023. 9(2): p. 266-279.
  26. Gallagher, C., et al., Alcohol and incident atrial fibrillation - A systematic review and meta-analysis. Int J Cardiol, 2017. 246: p. 46-52.
  27. National Academies of Sciences, Engineering, and Medicine. Review of Evidence on Alcohol and Health, 2025. Washington, DC: The National Academies Press. Available at:
  28. Piano, M. R. et al., Alcohol use and cardiovascular disease: A scientific statement from the American Heart Association. Circulation, 2025. 152(1): p. e7-e21.
  29. Cauley, J.A., et al., Studies on the association between alcohol and high density lipoprotein cholesterol: possible benefits and risks. Adv Alcohol Subst Abuse, 1987. 6(3): p. 53-67.
  30. Goel, S., A. Sharma, & A. Garg, Effect of Alcohol Consumption on Cardiovascular Health. Curr Cardiol Rep, 2018. 20(4): p. 19.
  31. Naimi, T.S., et al., Selection biases in observational studies affect associations between 'moderate' alcohol consumption and mortality. Addiction, 2017. 112(2): p. 207-214.
  32. Stockwell, T., et al., Do "moderate" drinkers have reduced mortality risk? A systematic eeview and meta-analysis of alcohol consumption and all-cause mortality. J Stud Alcohol Drugs, 2016. 77(2): p. 185-98.