Unywaji pombe na mwili wako
Unywaji wa pombe una kuathiri vipi kimwili? Inategemea na wewe upo vipi
Wanawake kwa ujumla ni ndogo kuliko wanaume na miili yao ina mafuta mengi na maji kidogo. Hii inamaanisha kuwa pombe katika kila kinywaji ambacho mwanamke anatumia itakaa zaidi mwilini mwake kuliko kiwango sawa katika mwili wa mwanaume, na atahisi athari ya pombe haraka zaidi (1, 2).
Miili ya wanawake pia huchakata pombe taratibu kuliko miili ya wanaume. Inachukua muda mrefu kwa pombe kutoka mwilini . Tofauti hizi zina mchango mkubwa katika namna ambavyo unywaji pombe unaweza kuwa na atharikwa afya ya wanaume na wanawake (3, 4). Watu hawana jinsia halisi na wale wanaobadilisha jinsia wanapaswa kushauriana na madaktari wao juu ya jinsi pombe inaweza kuwaathiri.
Jinsi mwili wako unavyochakata pombe inategemea na umri wako
Imebainika kuwa watoto na vijana huchakata pombe kwa namna tofauti na watu wazima kwa sababu miili yao bado inaendelea kukua. Kwa sababu hii, kunywa katika umri mdogo kunaweza kusababisha athari mbaya baadaye maishani (5, 6). Nchi nyingi zina sheria ambazo zinaweka kikomo cha umri halali chini ya unywaji ambao hairuhusiwi na vijana walio chini ya umri hawapaswi kunywa pombe (7).
Lakini umri pia huaathiri namna ambavyo watu wenye umri mkubwa huchakata pombe Kunywa huathiri wazee tofauti na watu wenye umri wa kati na wadogo. Tunapozeeka, tunapoteza uwezo wetu wa kuchakata pombe (9). Inaweza kukaa katika miili yetu kwa muda mrefu na kwa hivyo tunaweza kupata athari zake kwa njia tofauti.
Tunapozeeka, tuna uwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya kiafya ukilinganisha na vijana wenye umri mdogo kuwa na shida na matumizi ya pombe yanaweza kuchangia kupata matizo zaidi ya kiafya. Tuna uwezekano mkubwa pia wa tunaweza kutumia dawa ambazo zinaweza kuingiliana na pombe (10). Daima inashauriwa kushauriana na wataalamu wa afya kuhusu kunywa pombe na jinsi inaweza kutuathiri, haswa tunapokuwa wazee.
Saizi ya mwili na uzito wako ni muhimu
Kwa ujumla inachukua muda mrefu kwa watu wakubwa kuhisi athari ya kunywa kuliko watu wadogo. Ukubwa wa mwili na uzito huathiri jinsi pombe inavyochakatwa, haraka au polepole (11). Pia zinaathiri ni kwa muda gani unahisi athari ya pombe.
Licha ya tofauti hizi, kila mtu - awe mkubwa au mdogo, mwembamba au mzito - anahusika na athari za pombe na madhara kutokana na kunywa kupita kiasi.
Jinsi unavyoweza kuimudu pombe inategemea afya yako kwa ujumla
Jinsi unavyohisi baada ya kunywa inaweza kutegemea ikiwa wewe ni mzima au mgonjwa, na ikiwa unatumia dawa, na ni zipi. Watu ambao wana magonjwa au hali fulani wanaweza kushauriwa kupunguza kiasi cha kunywa au kutokunywa kabisa (12-15). Kama unapata matibabu, unatakiwa kumwona mtaalamu wa afya kupata ushauri kama unaweza kunywa pombe(12-15).
Dawa mara nyingi hujumuisha maonyo muhimu ambayo hushauri kutokunywa pombe, kwani kunaweza kuwa na mwingiliano ambao unaweza kuathiri jinsi unavyohisi, hali yako ya akili, na jinsi dawa itakavyokuwa na ufanisi (10).
Tabia za maumbile unazorithi zina jukumu katika jinsi pombe inaweza kukuathiri
Watu wengine hawawezi kuchakata pombe kwa ufanisi kwa sababu ya tofauti ya maumbile ambayo huathiri jinsi inachakatwa na miili yao (16, 17). Tofauti hii ya maumbile ni ya kawaida kati ya watu wa asili ya Kichina, Kijapani na Kikorea kuliko kati ya vikundi vingine (18). Hata ikiwa wana afya njema, watu ambao wana upungufu huu wanaweza kusukutika usoni wanapokunywa, na kujisikia wagonjwa na kizunguzungu hata baada ya kunywa pombe kidogo.
Historia ya familia na maumbile ya kurithi pia ni sehemu ya sababu ya watu wengine kukuza Matatizo ya Matumizi ya Pombe (AUD) au 'ulevi' (16,19). Hali hii inaweza kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwenye baadhi ya familia (20, 21). Watu ambao wanapata shida na unywaji wao au hawawezi kuacha wanapaswa kukutana na mtaalamu wa afya kwa ushauri na wanaweza kuhitaji matibabu.
Kutumia dawa hubadilisha uzoefu wako na unywaji pombe
Pombe hufanya kazi kwenye ubongo na mfumo wa fahamu , ambapo hutoa athari zake nyingi. Kiwango cha athari hizo hutegemea ni kiasi gani unakunywa, pamoja na umri wako, uzito, jinsia na mambo mengine yaliyojadiliwa katika sehemu hii.
Dawa za kulevya kama bangi, opiates, amphetamini na nyinginezo, iwe ni halali au haramu, pia hufanya kazi kwenye ubongo (22, 23). Zinanaweza kuingiliana na pombe na athari za pamoja inaweza kuwa mbaya na ni vigumu kuzitabiri (24). Kuchanganya dawa na pombe inaweza kuwa hatari na inaweza kusababisha kifo, kulingana na ni kiasi gani unakunywa na dawa unazotumia. Haupaswi kuchanganya pombe na dawa zilizoandikwa na daktari bila kushauriana na mtaalamu wa afya. Ni kweli, haupaswi kamwe kutumi dawa za kulevya haramu, lakini haswa iliyochanganywa na pombe.
Kula na kunywa huchangia jinsi mwili wako unachakata pombe
Sababu ya hii ni rahisi. Kula hupunguza kiwango ambacho pombe huingizwa ndani ya damu yako na jinsi unahisi athari zake haraka (11). Kuwa na maji mengi, kwa kunywa vinywaji visivyo na kilevi na maji, husaidia mwili wako kuchakata pombe na kuitoa nje ya mfumo wako baada ya kuchakatwa . Daima ni wazo nzuri kula wakati unakunywa na kunywa pombe na kuchanyanya na vinywaji vingine.
Lakini kula na kunywa vimiminika hakutakuzuia kulewa au kupunguza athari ambazo unywaji wa kupita kupita kiasi unaweza kuleta kwa mwili wako.
- Harvard Health Publishing. Alcohol's effects on the body. 2014; Available from:
- Thomasson, H.R., Gender differences in alcohol metabolism. Physiological responses to ethanol. Recent Dev Alcohol, 1995. 12: p. 163-79.
- Erol, A. and V.M. Karpyak, Sex and gender-related differences in alcohol use and its consequences: Contemporary knowledge and future research considerations. Drug Alcohol Depend, 2015. 156: p. 1-13.
- National Institute on Alcohol Abuse and Alcoholism (NIAAA). Women and alcohol. 2019; Available from:
- Spear, L.P., Effects of adolescent alcohol consumption on the brain and behaviour. Nat Rev Neurosci, 2018. 19(4): p. 197-214.
- Lees, B., et al., Effect of alcohol use on the adolescent brain and behavior. Pharmacol Biochem Behav, 2020. 192: p. 172906.
- International Alliance for Responsible Drinking (IARD). Minimum legal age limits. 2020; Available from:
- National Institute on Alcohol Abuse and Alcoholism (NIAAA). Older adults. 2020; Available from:
- Meier, P. and H.K. Seitz, Age, alcohol metabolism and liver diseases. Current Opinions in Clinical Nutrition and Metabolic Care, 2008. 11: p. 21026.
- National Institute on Alcohol Abuse and Alcoholism (NIAAA). Harmful interactions: mixing alcohol with medicines. 2014; Available from:
- Cederbaum, A.I., Alcohol metabolism. Clin Liver Dis, 2012. 16(4): p. 667-85.
- Puddey, I.B. and L.J. Beilin, Alcohol is bad for blood pressure. Clin Exp Pharmacol Physiol, 2006. 33(9): p. 847-52.
- Mental Health Foundation. Alcohol and mental health. 2020; Available from:
- Engler, P.A., S.E. Ramsey, and R.J. Smith, Alcohol use of diabetes patients: the need for assessment and intervention. Acta Diabetol, 2013. 50(2): p. 93-9.
- British Heart Foundation (BHF). Heart conditions and alcohol. 2020; Available from:
- Bierut, L.J., et al., A genome-wide association study of alcohol dependence. Proc Natl Acad Sci U S A, 2010. 107(11): p. 5082-7.
- Edenberg, H.J., The genetics of alcohol metabolism: role of alcohol dehydrogenase and aldehyde dehydrogenase variants. Alcohol Res Health, 2007. 30(1): p. 5-13.
- Iwahashi, K. and H. Suwaki, Ethanol metabolism, toxicity and genetic polymorphism. Addict Biol, 1998. 3(3): p. 249-59.
- Edenberg, H.J., J. Gelernter, and A. Agrawal, Genetics of Alcoholism. Curr Psychiatry Rep, 2019. 21(4): p. 26.
- Cservenka, A., Neurobiological phenotypes associated with a family history of alcoholism. Drug Alcohol Depend, 2016. 158: p. 8-21.
- Sanchez-Roige, S., A.A. Palmer, and T.K. Clarke, Recent Efforts to Dissect the Genetic Basis of Alcohol Use and Abuse. Biol Psychiatry, 2020. 87(7): p. 609-618.
- Volkow, N.D. and M. Morales, The Brain on Drugs: From Reward to Addiction. Cell, 2015. 162(4): p. 712-25.
- Koob, G.F. and N.D. Volkow, Neurobiology of addiction: a neurocircuitry analysis. Lancet Psychiatry, 2016. 3(8): p. 760-773.
- Singh, A.K., Alcohol Interaction with Cocaine, Methamphetamine, Opioids, Nicotine, Cannabis, and gamma-Hydroxybutyric Acid. Biomedicines, 2019. 7(1).
Una wasiwasi juu ya athari za kunywa kwenye mwili wako?
Ikiwa ni juu yako mwenyewe au mtu mwingine, tumia tathmini yetu ya kunywa kufahamu hatari.
Ikiwa wewe au mtu unayemjua ana kuwa na matokeo mapaya ya kunywa pompe, orodha yetu ya mitandao ya msaada ni mahali pazuri kuanza.